728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, May 18, 2017

    Kucheza Europa Ligi siyo mwisho wa dunia nyinyi


    London,England.

    MLINDA MLANGO Peter Cech amesema yeye pamoja na wachezaji wenzake wa Arsenal wataipa heshima inayostahili michuano ya Europa Ligi ikiwa watashindwa kuingia nne bora na kufuzu kucheza michuano ya klabu bingwa Ulaya msimu ujao.

    Cech,34, ameongeza kuwa kucheza michuano ya Europa Ligi siyo mwisho wa dunia na kusisitiza kuwa ikiwa wataangukia huko basi watakamua kikweli kweli kama wako klabu bingwa.

    Cech ametoa kauli hiyo hii ni baada ya Arsenal kuwa katika hatari kubwa ya kushindwa kufuzu michuano ya klabu bingwa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1998.

    Ili kufuzu nne bora Arsenal iliyo katika nafasi ya tano italazimika kuiombea mabaya Liverpool inayoshika nafasi ya nne ifungwe mchezo wake wa mwisho nyumbani Anfield dhidi ya Middlesbrough ambayo tayari imeshashuka daraja.

    Akifanya mahijiano na The
    Mirror,Cech amesema taji la Ulaya ni taji la Ulaya tu.Kila mtu anataka kucheza ligi ya mabingwa kuliko Europa Ligi .Lakini utaona kwamba vilabu vingi vikubwa vinaipa Europa Ligi heshima kwa sababu ni michuano ya Ulaya.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Kucheza Europa Ligi siyo mwisho wa dunia nyinyi Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top