Berlín,Ujerumani.
KWA NIA NJEMA kabisa Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Ujerumani,Joachim Low ameamua kuwaweka kando mastaa wake kwa kutowajumuisha kwenye kikosi cha wachezaji 23 cha nchi hiyo ambacho hivi karibuni kitaingia kambini kujiandaa na michuano ya kombe la mabara itakayofanyika mwezi ujao huko nchini Urusi.
Mastaa walioachwa ni pamoja na Toni Kroos,Thomas Muller na Mesut Ozil.Wengine ni Manuel Neuer, Mats Hummels na Marco Reus,Jerome Boateng, Mario Gomez, Mats Hummels, Sami Khedira,Mario Gotze,Benedikt Howedes na Julian Weigl.
Akizungumzia uwamuzi wa kuwaacha mastaa hao,Low amesema lengo ni kuwapa muda wa kutosha wa mapumziko ili wakusanye nguvu tayari kwa kulitetea kombe la dunia walilolitwaa mwaka 2014 nchini Brazil.
Katika hatua nyingine Low amewaongeza kikosini wachezaji wapya saba ili kuziba nafasi za mastaa aliowaacha.Wachezaji hao ni Kevin Trapp, Marvin Plattenhardt, Kerem Demirbay, Diego Demme, Lars Stindl, Sandro Wagner na Amin Younes.
Wachezaji hao wataungana na wachezaji kama Niklas Sule,Benjamin Henrichs na Timo Werner ambao tayari wameishaichezea Ujerumani mchezo mmoja mmoja.
Matthias Ginter, Shkodran Mustafi na Julian Draxler ndiyo wachezaji pekee waliotwaa kombe la dunia waliopata bahati ya kusalia kwenye kikosi cha Low.
Ujerumani imepangwa Kundi B pamoja na mataifa ya Cameroon,Chile na Australia.Kundi A, lina mataifa ya Urusi,Ureno,Mexico na New Zealand.
Kikosi Kamili
Makipa: Bernd Leno, Marc-Andre Ter Stegen, Kevin Trapp
Mabeki: Matthias Ginter, Jonas Hector,Benjamin Henrichs, Joshua Kimmich,Shkodran Mustafi, Marvin Plattenhardt,Antonio Rudiger, Niklas Sule
Viungo:Julian Brandt,Emre Can, Kerem Demirbay, Diego Demme,Julian Draxler, Leon Goretzka, Sebastian Rudy.
Washambuliaji:Leroy Sane, Lars Stindl, Sandro Wagner, Timo Werner, Amin Younes.
Michuano ya kombe la mabara itaanza Juni 17 na kufikia ukomo Julai 2.
0 comments:
Post a Comment