728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, May 19, 2017

    AFCON U17:Mali yafanya kweli na kuishusha Serengeti Boys kileleni mwa msimamo wa kundi B


    Libreville,Gabon.

    TIMU ya taifa ya Vijana ya Mali imeiondosha Serengeti Boys ya Tanzania kileleni mwa msimamo wa kundi B la michuano ya vijana ya AFCON ya umri wa chini ya miaka 17 baada ya Alhamisi usiku kuifunga Niger mabao 2-1 katika mchezo wa pili wa kundi hilo uliochezwa huko Stade de l'Amitié,jijini Libreville.

    Drame alianza kuipa uongozi Mali katika dakika ya 6 tu ya mchezo baada ya kuifungia bao safi la kuongoza akiwa ndani ya boksi la Niger.

    Katika dakika ya 35 vijana wa Niger waliamka na kufanikiwa kusawazisha kupitia kwa Habibou Sofiane aliyefunga bao safi kwa mkwaju wa adhabu.

    Bao hilo halikudumu sana kwani katika dakika kumi baadae yaani katika dakika ya 45,Mohamed Camara aliifungia Mali bao la pili na la ushindi.

    Ushindi huo umeifanya Mali ifikishe pointi 4 na mabao mawili sawa na Serengeti Boys lakini inakaa kileleni kutokana na herufi ya mwanzo ya jina (Alphabet).Mali inaanzia na herufi M wakati Tanzania inaanzia na herufi T.

    Pazia la michezo ya kundi B litafungwa siku ya Jumapili ambapo Serengeti Boys itakuwa ikivaana na Niger Mali ikipepetana na Angola. Serengeti Boys na Mali zinahitaji ushindi ama sare yoyote ile ziweze kufuzu hatua ya nusu fainali.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: AFCON U17:Mali yafanya kweli na kuishusha Serengeti Boys kileleni mwa msimamo wa kundi B Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top