Manchester,England.
USIKU wa kuamkia leo kulikuwa na kazi moja tu jijini Manchester.Kazi hiyo haikuwa nyingine bali ni kuwatunuku mituzo kama si mizawadi wachezaji waliofanya kweli wakiwa na jezi ya Manchester United kwa msimu wa 2016/17.
Kiungo Ander Herrera amehitimisha utawala wa miaka mitatu wa Mhispania mwenzake,David De Gea baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa msimu wa Manchester United.
Herrera mwenye umri wa miaka 27 ametwaa tuzo hiyo kwa tofauti ya kura 242 dhidi ya mlinzi,Antonio Valencia aliyeshika nafasi ya pili.Nafasi ya tatu imeshikwa na Zlatan Ibrahimovic.
Antonio Valencia ametwaa tuzo ya mchezaji bora chaguo la wachezaji huku Henrick Mkhitaryan akitwaa tuzo ya bao bora la msimu.Ni lile bao la maajabu la Scorpion Kick alilofunga mwezi Disemba dhidi ya Sunderland.
Axel Tuanzebe ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa kikosi cha akiba huku Angel Gomes ambaye ni mpya wa nyota wa zamani wa timu hiyo Luis Nani akitwaa tuzo ya mchezaji bora chipukizi.
0 comments:
Post a Comment