728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, May 16, 2017

    Marekebisho ya kanuni ligi kuu na ligi daraja la kwanza Tanzania Bara msimu wa 2017/18


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF),linazitangazia klabu zote zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2017/18 na zile za Ligi Daraja la Kwanza(FDL) msimu wa 2017/18 kwamba kipindi hiki ni cha kuwasilisha maoni na mapendekezo mbalimbali kuhusu marekebisho ya kanuni za ligi husika.

    TFF inaagiza klabu zote -kwa nafasi walizonazo kama wanafamilia ya mpira wa miguu, kuwasilisha mapendekezo na maoni kuhusu marekebisho yakatiba kwa njia ya kuyatuma kupitia anwani za sanduku la Barua 1574,Dar es Salaam au barua pepe tplb.tplb@yahoo.com au yaletwe moja kwa moja ofisi za Bodi ya Ligi au
    TFF.


    Maoni hayo tayafanyiwa kazi na Bodi ya Ligi kabla ya kupelekwa kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji kabla ya kuanza msimu husika wa mashindano baada ya kupita msimu uliopita.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Marekebisho ya kanuni ligi kuu na ligi daraja la kwanza Tanzania Bara msimu wa 2017/18 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top