728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, May 11, 2017

    Maandalizi Ligi Kuu:Njombe Mji yaanza usajili rasmi,yaliongeza nguvu pia benchi lake la ufundi.


    Mwandishi Wetu,Njombe.

    TIMU ya Njombe Mji ambayo msimu ujao itashiriki kwa mara ya kwanza ligi kuu ya soka ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) imeanza rasmi maandalizi ya kukisuka upya kikosi chake tayari kwa mikikimiki ya ligi hiyo kubwa hapa nchini kwa kufungua milango kwa wachezaji wanaotaka kusajiliwa na timu hiyo kwenda kujaribu bahati yao mkoani humo.

    Akifanya mahojiano na Mtandao huu,Afisa habari wa Njombe Mji,Solanus Mhagama amesema usajili huo uliodhamiria kuifanya Njombe Mji itishe ligi kuu msimu ujao utakuwa ni wa awamu mbili.

    Awamu ya kwanza itafanyika kuanzia Mei 15 mpaka 20 na utahusisha wachezaji ambao hawajapendekezwa na benchi la ufundi.Wachezaji hao ni wale watakaokwenda mjini hapo bila ya kupata mwaliko kutoka kwenye benchi la ufundi la timu hiyo.Wachezaji hao wametakiwa kujitegemea nauli na mambo mengine.

    Usajili wa awamu ya pili utaanza Mei 20 na ni ule utakaohusisha wachezaji waliopendekezwa na benchi la ufundi pamoja na wale waliopandisha timu hiyo daraja.Wachezaji hao watagharamiwa nauli.

    Wakati huohuo Mhagama ameongeza kuwa kamati ya utendaji ya Njombe Mji kupitia kwa Mwenyekiti Wake,Erasto Mpete imeliongezea nguvu benchi lake la ufundi kwa kumtangaza Mlage Kabange kuwa kocha wake msaidizi huku nafasi ya Kocha Mkuu ikiendelea kushikiliwa na Ahmed Banyai.Damian Mkule ataendelea na jukumu lake la kuwa Meneja wa timu.Nafasi ya kocha wa makipa itazibwa baadae.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Maandalizi Ligi Kuu:Njombe Mji yaanza usajili rasmi,yaliongeza nguvu pia benchi lake la ufundi. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top