728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, May 11, 2017

    Serengeti Boys yapenya mtihani wa kughushi umri


    Libreville, Gabon.

    TIMU ya taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys imewashiwa taa ya kijani na shirikisho la soka barani Afrika,CAF  kuendelea na maandalizi yake ya kujiwinda na michuano ya vijana itakayofanyika baadae wiki hii nchini Gabon baada ya wachezaji wake kubainika kuwa hawajaghushi umri.

    Akiongea kutoka nchini Gabon,Mwenyeki wa kamati ya soka la vijana,Ayubu Nyenzi amesema juzi Jumanne wachezaji watano wa Serengeti Boys walichukuliwa na kwenda kufanyiwa kipimo cha MRI ili kubaini kama wameghushi umri ama la.

    Majibu yaliyotolewa yameonyesha kwamba kati ya wachezaji wote watano waliofanyiwa vipimo hakuna hata mchezaji mmoja wa Serengeti Boys aliyebainika kuwa na umri mkubwa zaidi ya miaka 17.

    Vipimo vya MRI hufanywa ili kubaini kama wachezaji wameghushi umri ama la na inapobainika kuwa mchezaji ameghushi umri basi mchezaji pamoja na timu yake huondolewa kwenye mashindano.

    Nyenzi ameongeza kuwa zoezi la upimaji wa kubaini umri litakuwa ni endelevu na litazihusu timu zote ambazo zitashiriki michuano ya vijana itakayoanza kutimua vumbi Jumapili Mei 14.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Serengeti Boys yapenya mtihani wa kughushi umri Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top