728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, May 11, 2017

    Hizi hapa habari kubwa za usajili kutoka barani Ulaya kwa Alhamisi ya leo Mei 11


    Bellerin: Albert Botines ambaye ni wakala wa mlinzi wa kulia wa Arsenal,Hector Bellerin amekiri kuwa amepokea ofa kwa ajili ya mteja wake huyo lakini si kutoka katika klabu yake ya zamani ya Barcelona kama ilivyoripotiwa hapo kabla. Bellerin,23,amekuwa akihusishwa na mpango wa kutaka kuondoka Arsenal katika siku za hivi karibu hasa baada ya Kocha Arsene Wenger kushindwa kuweka wazi hatima yake kama ataondoka ama atabaki klabuni hapo.


    De Roon:Everton imeelezea nia yake ya kutaka kumsajili kiungo wa Middlesbrough, Mholanzi Marten de Roon limeandika gazeti la Daily Mail.De Roon,26,ameonyesha kiwango bora tangu alipojiunga na Middlesbrough msimu uliopita akitokea Atalanta ya Italia.Dau la £12m limedauwa kuwa litaishawishi Middlesbrough kumwachia kiungo huyo wa nguvu.


    Sandro;Kocha wa Everton,Mdachi Ronald Koeman amepewa ruhusa na klabu hiyo kuanza mipango ya kumsajili straika wa Malaga,Sandro pamoja na kiungo wa Ajax,Davy Klaassen.Limeandika The Mirror.Sandro ambaye ni nyota wa zamani wa Barcelona amedaiwa kuwa na thamani ya £5 huku dau £20m likidaiwa kuwa litaishawishi Ajax kumwachia Klaassen ambaye ni nahodha wake.


    Coutinho:Kocha wa Liverpool,Jurgen Klopp amesisitiza kuwa kiungo wake mahiri Philippe Coutinho atabakia klabuni hapo licha ya kutakiwa kwa udi na uvumba na klabu ya Barcelona ya nchini Hispania.Mwezi Januari Coutinho,24,alisaini mkataba wa miaka mitano wa kusalia Anfield lakini hilo bado halijaikatisha tamaa Barcelona.



    Hart:Kipa wa Manchester City anayecheza kwa mkopo Torino ya Italia,Joe Hart huenda kwa mara nyingine akabiliwa na changamoto ya kupata timu mpya msimu ujao baada ya matakwa yake ya mshahara pamoja na ada lake la uhamisho kuzitisha timu nyingi barani Ulaya.Manchester City inataka dau la £30m huku Hart mwenyewe akitaka alipwe mshahara wa £120,000 kwa wiki.(Manchester Evening News)



    Stam:Kocha wa Reading,Mdachi Jaap Stam amesema hajui kama atakuwa klabuni hapo msimu ujao.Stam ametoa kauli hiyo baada ya hivi karibu kuanza kunyatiwa na vilabu vya ligi kuu England kutokana na kuiwezesha Reading kushika nafasi ya tatu Championship.

    Masip:Kipa wa Barcelona,Jordi Masip amekataa ofa ya kujiunga na Red Bull Salzburg ya Australia.Ripoti kutoka RAC1.Masip ambaye ni kipa chaguo la tatu Barcelona anasubiri kuona kama miamba hiyo itampa mkataba mpya pindi ule wa sasa utakapoisha mwezi ujao


    Asensio:Marco Asensio ameishtua klabu yake ya Real Madrid baada ya kudai kuwa atafikiria kuhamia Liverpool ama Arsenal ikiwa ataendelea kukosa namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Zinedine Zidane. Limeandika Diario Gol.Mpaka sasa Asensio ameicheza Real Madrid michezo 19 tangu alipojiunga nayo Disemba 2014 akitokea Mallorca.


    Coentrao:Galatasaray imeonyesha nia ya kutaka kumsajili beki wa kushoto asiye na nafasi klabuni Real Madrid,Mreno Fabio Coentrao mwenye mkataba mpaka 2019.Coentrao,29,anataka kuondoka Real Madrid baada ya msimu huu kucheza michezo miwili pekee. Mbali ya Galatasaray,Sporting Lisbon pia imedaiwa kuwa na mpango wa kutaka kumsajili beki huyo anayesota benchi Santiago Bernabeu.

    Mboula:West Ham imeripotiwa kuwa imefungua mazungumzo na Barcelona kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wake kinda Jordi Mboula.Mboula,18, anayefananishwa kiuchezaji na nyota wa zamani wa Arsenal,Thierry Henry amedaiwa kuwa na thamani ya £4.1m.Limeandika The Daily Star


    Morata:Chelsea inahofia kufungua mazungumzo na Real Madrid kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji Mhispania,Alvaro Morata kwa kuhofia huenda nyota wake wawili Eden Hazard na Thibaut Courtois wakahusishwa kwenye dili hilo.Limeandika Evening Standard.





    Alves:Meneja wa Chelsea, Antonio Conte anafikiria kufanya usajili wa kushitukiza kwa kumsajili beki wa kulia wa Juventus,Dani Alves.Limeandika Daily Express. Alves,34,amemvutia Conte baada ya hivi karibuni kuonyesha kiwango bora ikiwa sambamba na kuisaidia Juventus kufuzu finali ya michuano ya klabu bingwa Ulaya.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Hizi hapa habari kubwa za usajili kutoka barani Ulaya kwa Alhamisi ya leo Mei 11 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top