Southampton,England.
ARSENAL imefanikiwa kuirejesha Manchester United mpaka nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka nchini England baada ya usiku huu ikiwa ugenini St.Mary's kuwafunga wenyeji wao Southampton kwa mabao 2-0 kwenye mchezo wa kiporo.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi John Moss ilishuhudiwa Arsenal ikijipatia mabao yake yote kipindi cha pili kupitia kwa Alexis Sanchez aliyefunga bao la kwanza katika dakika ya 60 kabla ya Olivier Giroud kuongeza la pili kwa kichwa katika dakika ya 84.
Ushindi huo umeifanya Arsenal ichupe mpaka nafasi ya tano baada ya kufikisha pointi 66.Pointi moja zaidi ya Manchester United ambayo sasa imeshuka mpaka nafasi ya sita ikiwa na pointi zake 65.
Aidha katika mchezo huo Arsenal ilipata pigo baada ya kulazimika kufanya mabadiliko ya lazima kufuatia winga wake Alex Oxlade Chamberlain kupata jeraha la misuli ambalo linahofiwa kuenda likamweka nje ya dimba mpaka mwisho wa msimu.
0 comments:
Post a Comment