728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, May 11, 2017

    Real Madrid yaifuata Juventus fainali ligi ya mabingwa Ulaya.


    Madrid,Hispania.

    REAL MADRID imeungana na Juventus kufuzu hatua ya nusu finali ya michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya baada ya kuwatupa nje wapinzani wao wa jadi Atletico Madrid licha ya kufungwa mabao 2-1 kwenye mchezo wa marudiano wa hatua ya nusu fainali uliochezwa usiku huu kwenye uwanja wa Vicente Calderon jijini Madrid.

    Katika mchezo huo uliochezeshwa na Mwamuzi,Cuneyt Cakir kutoka nchini Uturuki ilishuhudiwa wenyeji Atletico Madrid wakijipatia mabao yao mwanzoni mwa kipindi cha kwanza katika dakika za 11 na 15 kupitia kwa Saul Niguez na Antoine
    Griezmann aliyefunga kwa mkwaju wa penati baada ya Fernando Torres kuangushwa ndani ya boksi na Rafael Varane.Bao la Real Madrid limefungwa na Fransesco Isco Alcaron katika dakika ya 42.


    Real Madrid inafuzu fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-2.Ikumbukwe Real Madrid ilishinda mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza uliochezwa dimbani Santiago Bernabeu Jumanne iliyopita.

    Fainali ya klabu bingwa barani Ulaya safari hii itachezwa Jumamosi ya Juni 3 huko nchini Wales kwenye dimba la uwanja wa Cardiff na ikiwa Real Madrid watatwaa ubingwa huo basi watakuwa wameweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kuutwaa ubingwa huo mara mbili mfululizo.Real Madrid ndiyo mabingwa watetezi.


    Vikosi:

    Atletico Madrid:Oblak, Gimenez (Thomas 57), Savic, Godin,Filipe Luis, Koke (Correa 76), Gabi, Saul,
    Carrasco, Torres (Gameiro 56), Griezmann.

    Real Madrid:Navas, Danilo, Sergio Ramos, Varane, Marcelo,Kroos, Casemiro (Lucas 76), Modric, Isco
    (Morata 87), Benzema (Marco 77), Ronaldo.

    Mwamuzi:Cuneyt Cakir 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Real Madrid yaifuata Juventus fainali ligi ya mabingwa Ulaya. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top