728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, May 10, 2017

    Yanga SC yataka mchezo wake dhidi ya Mbeya City uchezwe usiku


    Paul Manjale,Dar Es Salaam.

    MABINGWA watetezi wa taji la kuu ya soka ya Vodacom Tanzania Bara (VPL),Yanga SC wameiandikia barua bodi ya ligi kuomba mchezo wao wa Jumamosi hii dhidi ya Mbeya City uchezwe saa 12:00 jioni badala ya saa 10:00 jioni kama ilivyozoeleka kwa michezo mingi ya ligi hiyo kuchezwa katika muda huo.

    Akieleza sababu ya kutaka mchezo huo ubadilishwe muda,Katibu mkuu wa Yanga SC,Charles Boniphase Mkwasa amesema wameomba mchezo huo uchezwe saa 12:00 kwa kuwa siku hiyo ya Jumamosi kutakuwa na mashindano ya kanda ya tano ya riadha ya vijana wa chini ya miaka 18 kwa nchi za Afrika Mashariki na kati kwenye uwanja mkubwa wa Taifa hivyo haitakuwa busara kuwa na michezo miwili kwa wakati mmoja.

    Sababu nyingine ambayo Mkwasa ameitoa ni kuwa hali ya hewa jijini la Dar Es Salaam kwa sasa imekuwa siyo rafiki sana kutokana na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha jijini humo hivyo wameamua kuomba mchezo huo usogezwe muda ili kutoa nafasi kwa uwanja kuwa katika hali nzuri.

    Yanga SC inaingia kwenye mchezo wa Jumamosi ikihitaji kushinda mchezo wake dhidi ya Mbeya City ili iweze kujitengenezea mazingira mazuri ya kuutetea ubingwa wake iliyoutwaa msimu uliopita.

    Yanga SC iko kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ikiwa imejikusanyia pointi 62 sawa na wapinzani wao Simba SC lakini vijana hao wa Jangwani wako juu kutokana na kuwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na ushindi katika michezo yao miwili kati ya mitatu iliyobakia utaipa ubingwa wa tatu mfululizo.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Yanga SC yataka mchezo wake dhidi ya Mbeya City uchezwe usiku Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top