728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, April 07, 2017

    Startimes kuonyesha kombe la dunia 2018



    Shirikisho la soka Dunia FIFA limetoa haki ya kurusha matangazo ya michuano ya fainali ya kombe la Dunia yatakayofanyika Russia mwaka 2018 kwa Starstimes kwa nchi za kusini mwa jangwa la SAHARA.

    Meneja masoko wa Starstimes Felix  Awino amesema watajitahidi kurusha matangazo bora ya fainali za kombe la dunia kwa wateja wao kwa kiwango cha juu huku mkuu wa bishara wa  FIFA Philippe Le Floc’h  akisema wanayofuraha kufanya ushirika na STARSTIMES kwani utasaidia kufikisha matangazo ya soka kwa mashabiki wegi wa soka Barani Afrika.

    Nchi 42 kusini mwa Jangwa La Sahara, zitapata matangazo hayo  kutoka Starstimes huku pia wakihusika kuonyesha fainali mbalimbali za FIFA, kama vile, fainali za kombe la dunia la FIFA la vijana  wenye umri chini ya miaka 17 na 20, fainali za kombe la Dunia la soka ya Ufukweni,fainali za kombe la shirikisho,fainali za kombe la dunia kwa wanawake wenye umri chini ya miaka 17 na 20 za mwaka 2018 na fainali zenyewe za  kombe dunia la FIFA nchini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Startimes kuonyesha kombe la dunia 2018 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top