728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, April 07, 2017

    SIRI:N'Golo Kante afichua kwanini aliitosa Arsenal na kutua Chelsea


    London,England.

    KIUNGO nyota wa Chelsea Mfaransa,N'Golo Kante amefichua kwanini alikataa kuhamia Arsenal mwishoni mwa msimu uliopita licha ya miamba hiyo ya Emirates kuonyesha nia ya kuitaka saini yake.

    Kante,26, amefichua kwamba alikataa ofa ya kujiunga na Arsenal inayofundishwa na Mfaransa,Arsene Wenger kwa kuwa haikuonyesha jitihada kubwa za kumuhitaji.

    "Arsenal walionyesha nia ya kunihitaji lakini nia yao haikuwa kubwa kama iliyoonyeshwa na vilabu vingine ndiyo maana nikaamua kuachana nao na kuamua kutua Chelsea" Kante ameiambia Sky Sports 

    Kante alijiunga na Chelsea Juni mwaka 2016 kwa dau la £30m akitokea kwa mabingwa watetezi wa ligi kuu England,Leicester City ambalo nao walimsajili kutoka Caen ya Ufaransa kwa dau la £7m.

    Akiwa na Chelsea tayari Kante anatajwa kuwa kiungo bora zaidi wa ulinzi ligi kuu England huku pia akipigiwa chapuo la kuibuka kinara kwenye kinyang'anyiro cha kumsaka mchezaji bora wa msimu.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SIRI:N'Golo Kante afichua kwanini aliitosa Arsenal na kutua Chelsea Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top