728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, April 06, 2017

    Serengeti Boys yawasili salama nchini Morocco


    Casablanca,Morocco.

    TIMU ya taifa ya Tanzania ya vijana chini ya miaka 17,Serengeti Boys imewasili salama jioni ya leo huko Casablanca nchini Morocco.

    Kocha mkuu wa timu hiyo,Bakari Shime "Mchawi Mweusi" amesema vijana wake wamewasili salama kwenye mji wa Casablanca ambapo baada ya mapumziko ya muda mfupi watasafiri kwa basi kwa umbali wa masaa mawili kuelekea katika mji wa Rabat ambako wataweka kambi ya wiki tatu kujiwinda na michuano ya vijana ya Afrika,AFCON itakayoanza Mei 14 huko nchini Gabon.

    Shime ameongeza kuwa baada ya kufika mjini Rabat vijana hao watapewa mapumziko mafupi ili kupunguza uchovu wa safari kabla ya Ijumaa jioni kuanza programu yao ya mazoezi.

    Ikiwa mjini Rabat,mbali ya kufanya mazoezi pia Serengeti Boys itapata nafasi ya kucheza michezo kadhaa ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya mataifa ya Misri na Morocco.

    Serengeti Boys iliondoka nchini jana Jumatano saa 10:15 jioni kwa ndege ya shirika la ndege la Emirates ikipitia Dubai,Falme za Kiarabu kabla ya jioni ya leo kuwasili nchini Morocco.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Serengeti Boys yawasili salama nchini Morocco Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top