728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, April 03, 2017

    Serengeti Boys watoka suluhu na Ghana , Wawaaga vizuri Watanzani



    Faridi Miraji , Dar es salaam.                       


    Mechi hii imepigwa jioni ya leo katika uwanja wa Taifa na kushuhudia wenyeji Serengeti Boys wakifanikiwa kulinda rekodi yao ya kutofungwa nyumbani.
    Mabao ya Serengeti yalifungwa  kipindi cha pili katika dakika kumi za nyongeza kupitia kwa Assad Juma aliyekwamisha mkwaju wa penati dakika ya 95 na Mukhsin Malima aliyefunga dakika ya mwisho ya nyongeza.
    Ghana walionekana kutawala kipindi cha kwanza walipata bao lao kwanza kupitia Sulley Ibrahim aliyeachia mkwaju mkali nje ya eneo la kumi nane na kumzidi kipa wa Serengeti Ramadhan Kabwili.


    Walikuwa ni Ghana tena waliopata bao la pili baada ya kipindi cha pili kuanza. Kiungo mkabaji wa Serengeti Boys, Ally Ng’anzi alifanya makosa ya kumchezea rafu Mensah ndipo mwamuzi alipoamuru pigo huru nje kidogo ya eneneo la hatari la Tanzania.
    Mkwaju wa Mensah ulikwenda moja kwa moja katika paa la lango la Serengeti Boys huku kipa Ramadhan akichupa bila mafanikio.
    Baada ya mchezo huu, Serengeti Boys wanatarajiwa kuelekea Morocco kwa ajili ya kambi ya mwezi mmoja kujiandaa na maandalizi ya mwisho ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Gabon.Serengeti Boys mwendo ni Gabon mpaka kombe la Duniani
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Serengeti Boys watoka suluhu na Ghana , Wawaaga vizuri Watanzani Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top