James Eduma,Pemba.
Baadhi ya Mashabiki wa timu ya Simba wanao ishi kisiwani Pemba wamesema wamekata tamaa ya kuibuka na ubingwa wa ligi kuu ya Zanzibar mwaka huu, baada ya kupoteza mchezo wao wa hapo jana dhidi ya Kagera Suger uliochezwa kwenye uwanja wa Kaitaba Bukoba na Wekundu hao kulala kwa kipigo cha magoli 2-1.
Mmoja wa Mashabiki hao Khallef Salim Abdalla wa Ndagoni Chake Chake Pemba amesema baada ya Yanga kushinda mchezo wao dhidi ya Azam FC hapo juzi na wao kufungwa na Kagera hapo jana hawana njia nyengine ya kuwazuia Yanga wasichukue ubingwa.
0 comments:
Post a Comment