PSG imetwaa kwa mara ya nne mfululizo ubingwa wa kombe la ligi la nchini Ufaransa maarufu kama Coupe de la Ligue (Sawa na Capital One Cup kwa Uingereza) baada ya usiku huu kuifumua AS Monaco kwa mabao 4-1 katika mchezo mkali wa fainali uliochezwa huko Stade des Lumieres,jijini Lyon.
Shujaa katika mchezo huo alikuwa ni winga Angel Di Maria aliyefunga bao moja na kupika mengine matatu yaliyofungwa na Julian Draxler aliyefunga bao moja pamoja na Edinson Cavani aliyefunga mabao mawili.Bao la AS Monaco limefungwa na Thomas Lemar.
0 comments:
Post a Comment