728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, April 04, 2017

    Bayern Munich kuitibulia Manchester United kwa Rick Karsdorp


    Rick Karsdorp (kulia) akimdhibiti Antony Martial wa Manchester United


    Munich,Ujerumani.

    BAYERN MUNICH ni kama imeamua kuitibulia Manchester United kwenye mbio za kuitaka saini ya beki mahiri wa kulia wa Feyenoord Mholanzi,Rick Karsdorp hii ni baada ya kuripotiwa pia kuingia kwenye mbio hizo.

    Kwa mujibu wa gazeti la De Telegraaf la nchini Uholanzi,habari zinasema Bayern Munich ambayo awali haikutajwa kuwemo kwenye mbio za kumuwania beki huyo mwenye umri wa miaka 20 sasa imedandia mbio hizo kwa mbele na imeripotiwa kuwa tayari kutoa kitita cha Euro Milioni 20 kwa ajili ya kumnasa beki huyo aliyetajwa sana Old Trafford baada ya kuwa mwiba mkali kwa washambuliaji wa Manchester United kwenye michezo ya hatua ya makundi ya michuano ya Europa Liga.

    Bayern Munich inamuona Karsdorp ,20, kuwa mbadala wa muda mrefu wa beki na nahodha wake, Phillip Lahm anayetarajiwa kustaafu mwishoni mwa msimu huu.

    Karsdorp ni mmoja kati ya mastaa wanaofanya vizuri kwenye kikosi cha Feyenoord na ameripotiwa kuwa na mkataba na miamba hiyo ya Rotterdam mpaka mwaka 2020. 



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Bayern Munich kuitibulia Manchester United kwa Rick Karsdorp Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top