728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, April 04, 2017

    MAKALA:Wanafiki wa soka tubuni na muombeni msamaha Juma Kaseja kimoyomoyo


    Chiki Mchoma,Dar Es Salaam. 

    Kama kuna kiumbe ambacho kwa wiki kadhaa kuelekea Mechi ya Simba dhidi ya Kagera Sugar kiliishi kwa kutukanwa na kujengewa dhana mbaya ni kiumbe kilichopewa jina la Juma na Wazazi wake wa Ukoo wa Kaseja uliotamalaki kule Ujiji Kigoma. 

    Kila mnafiki wa Soka la Bongo alijenga dhana kuwa Kaseja ni Simba damu... Eti Bora akose Kula sio Kukosa kuiona Simba ikishinda hasa yeye Akiwa golini upande wa Timu inayoshambuliwa na Simba. 

    Wanafiki wa Soka la Bongo hawakuishia hapo... Walitaka tuamini pia kuwa JUMA K. JUMA amepewa mlungula na Simba ili afungishe timu yake ya Kagera Sugar.. Leo hii wamebaki kimyaa kama kawaida ya Wanafiki. 

    Fikiria iwapo JUMA K. JUMA angefungwa mechi ile...

    Tena Fikiria iwapo JUMA K. JUMA angefungwa goli kama alilofungwa Manyika Jr na Mussa Mgosi akiidakia Simba dhidi ya Mtibwa pale Jamhuri Morogoro. 

    Au unakumbuka Goli alilofungwa Victor Valdez na Antonio Valencia kwenye Mechi ya Hivi karibuni akiidakia timu yake ya BORO dhidi ya MAN U kwenye EPL??... Kumbuka Valdez alikuwa Man U kabla ya kuelekea Boro. 

    Umewahi kuwaza je JUMA K. JUMA angewekwa fungu gani katika Soka la Wanafiki wa Soka la Bongo??

    Umewahi kuhisi ni kwa kiasi gani angevunjiwa heshima na Utu wake yeye na Familia yake?? 

    Umewahi kuhisi ni Mangapi yangeandikwa kwenye Magazeti yetu mengi yaliyojaa Ushabiki wa Simba na Yanga?? 

    Umewahi kuhisi ni kwa kiasi gani Simu yake ingejaa Meseji za Kejeli na Uzushi na Udhalilishaji dhidi yake na familia yake?? 

    Umewahi kuhisi Mitandaoni angepewa jina gani jipya la Kejeli au angechafuliwa kiasi gani kiasi cha kumuathiri yeye na familia yake Kisaikolojia?? 

    Je, wewe binafsi ulimuweka kwenye fungu gani JUMA K. JUMA kuelekea mchezo huo dhidi ya Simba?? 

    Kama ulimjengea dhana mbaya basi nenda haraka UKATUBU KWA MUUMBA WAKO ALIYESEMA DHANA NI DHAMBI KUBWA.

    PIA CHUKUA DAKIKA CHACHE KUMUOMBA JUMA K. JUMA MSAMAHA KIMOYO MOYO.

    Leo unajisikiaje unapomuona JUMA K. JUMA anaonekana Shujaa wa Hisia zake na Nafsi yake na Kocha wake Mecky Mexime aliyemuamini na Kumhakikishia kupambana na Hisia za WANAFIKI WA SOKA LA BONGO KWA VITENDO WAZI.

    Kama kuna mtu Anastahili Sifa zilizopitiliza kwa Mafanikio ya JUMA K. JUMA kwenye Mechi dhidi ya Simba ni Kocha Mwenye Elimu Kamili ya Mpira na Mzoefu wa Soka la Kinafiki la Bongo ambaye ni Kepteni wa Zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania Mecky Mexime. 

    Hongera Sana zaidi ya Sana Kocha Mecky Mexime... Hakika umemtendea haki Golikipa wako naye ametekeleza wajibu wake ipasavyo na Amekutendea haki kwa kutekeleza uliyomuagiza kufanya. 

    Bila Mecky Mexime kuamua kufunga masikio na kupuuzia kelele za *WANAFIKI WA SOKA LA BONGO* pengine JUMA K. JUMA asingecheza mechi dhidi ya Simba na hivyo kumfanya azidi kuathirika zaidi Kisaikolojia. 

    *HONGERA KOCHA MEXIME WEWE NI KOCHA AMBAYE UMEBOBEA KWENYE WELEDI WA UFUNDISHAJI.*

    *HONGERA JUMA K. JUMA WEWE NI GOLIKIPA MAHIRI NA MWENYE WELEDI WA KAZI YAKO.*



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAKALA:Wanafiki wa soka tubuni na muombeni msamaha Juma Kaseja kimoyomoyo Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top