728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, April 08, 2017

    Ataka AFCON ifanyike kila baada ya miaka minne


    Cairo,Misri.

    RAIS mpya wa shirikisho la vyama vya soka barani Afrika CAF,Mmadagscar,Ahmad Ahmad amesema atazungumza na wataalamu wa mchezo huo wa ndani na nje ya Afrika ili kuona kama michuano ya mataifa huru ya Afrika maarufu kama AFCON iendeleee na utaratibu wake wa sasa wa kufanyika kila baada ya miaka miwili miwili ama iwe inafanyika kila baada ya miaka minne minne.

    Ahmad ambaye aliingia madarakani mwezi uliopita baada ya kumng'oa aliyekuwa kiongozi wa muda mrefu wa shirikisho hilo,Issa Hayatou kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika huko Addis Ababa‚Ethiopia amesema yuko tayari kubadili muda wa sasa wa michuano hiyo kutoka miaka miwili mpaka miaka minne kama ilivyo kwa michuano ya Copa Amerika,Euro na kombe la dunia.

    AFCON ni michuano muhimu sana Afrika na hata duniani kote,ni michuano ya tatu kwa ukubwa.Nitafungua mijadala (majadiliano) na nitaomba ushauri kwa watu mbalimbali walioko kwenye mpira,wanahabari,maafisa ili kujadili kuona kama kuna hitaji la kusogeza mbele muda wa michuano hiyo.

    Niko tayari kusikiliza maoni ya wengine.Mimi siyo mtu ninayefanya maamuzi peke yangu.Ni juu ya watu kuamua kuhusu mpango huo.Amesema Ahmad.

                  

    Ahmad anaona kwamba kuisogeza mbele michuano hiyo na kuifanya iwe inafanyika kila baada ya miaka minne kutapunguza presha kwa vilabu hasa katika kutoa ruhusa kwa wachezaji wao.Ahmad ameongeza kuwa itavutia hata wachezaji wenye tabia za kuidengulia michuano hiyo.Pia itaongeza thamani na mvuto wa michuano hiyo




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Ataka AFCON ifanyike kila baada ya miaka minne Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top