Girabola,Angola.
TAKRIBANI mashabiki 17 wa soka nchini Angola wameripotiwa kufa na wengine 76 kujeruhiwa katika mchezo wa ligi kuu ya nchi hiyo uliovikutanisha vilabu vya Santa Rita de Cassia na Recreativo de Libolo jana Ijumaa kwenye uwanja wa Estadio Municipal 4 de Janeiro ulioko kwenye mji wa Uige.
Chanzo cha maafa hayo kimedaiwa kusababishwa na kukanyagana ambapo mashabiki waliokuwa nje ya uwanja huo walivunja geti na kuingia kwa nguvu.Sehemu kubwa ya mashabiki waliokufa wakiripotiwa kuwa ni watoto.
Recreativo de Libolo kupitia mtandao wake imesema imesikitishwa na maafa hayo makubwa na kuongeza maafa hayo ni makubwa kuwahi kulikumba soka la Angola.
0 comments:
Post a Comment