Dar Es Salaam,Tanzania.
LIGI kuu ya Vodacom Tanzania Bara maarufu kama VPL inatarajiwa kuendelea tena leo kwa michezo minne ya ligi hiyo kuchezwa katika viwanja vinne tofauti hapa nchini.
Maafande wa Ruvu Shooting watakuwa mwenyeji wa Azam FC huko Mlandizi,Pwani.Stand United watakuwa nyumbani Kambarage Shinyanga kupepetana na Majimaji FC kutoka Songea.
Mabingwa wa zamani wa ligi hiyo Simba SC watakuwa Uwanja wa Uhuru kuwaalika maafanye wa Tanzania Prisons kutoka Mbeya.Ikiwa Simba SC watashinda mchezo wa leo watawaengua watani wao Yanga na kurejea kileleni.
Yanga hawatashuka dimbani wikendi hii kwenye michezo ya ligi kuu kwani hapo kesho Jumapili watakuwa na kibarua kigumu pale watakapokuwa wageni wa Ngaya ya Comoro kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika.
Mchezo wa mwisho leo hii utapigwa huko Nangwanda Sijaona,Mtwara,ambapo Ndanda FC watakuwa wenyeji wa Toto Africans ya Mwanza.
Ratiba Kamili
Ruvu Shooting v Azam FC
Stand United v Majimaji FC
Simba SC v Tanzania Prisons
Ndanda FC v Toto Africans
0 comments:
Post a Comment