London,England.
BAADA ya kuambulia vichapo viwili mfululizo kutoka kwa Watford na kisha baadae Chelsea hatimaye Arsenal leo imeona mwezi baada ya kuilaza Hull City kwa bao 2-0 nyumbani Emirates.
Alexis Sanchez alianza kuifungia Arsenal bao la kwanza katika dakika ya 33 baada ya kutokea piga nikupige langoni kwa Hull City.
Katika dakika ya 92 Alexis Sanchez aliiandikia Arsenal bao la pili kwa mkwaju wa penati baada ya beki wa Hull City,Clucas kuunawa mpira wa kichwa uliopigwa na Lucas Perez.
0 comments:
Post a Comment