Dar Es Salaam,Tanzania.
HATIMAYE Simba SC imerejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu bara baada ya jioni ya leo kuwalaza Maafande wa Tanzania Prisons kwa mabao 3-0 ,Uwanja wa taifa,Dar Es Salaam.
Juma Liuzio aliifungia Simba SC bao la kwanza katika dakika ya 18 akiuwahi mpira wa krosi uliopigwa na Jean Pierre Bokungu na kushindwa kuondolewa kwa wakati na walinzi wa Tanzania Prisons.
Ibrahim Ajib aliiongezea Simba SC bao la pili dakika ya 28 akimalizia kazi nzuri ya Mrundi Laudit Mavugo aliyewazidi maarifa walinzi wa Tanzania Prisons na kutoa pasi kwa mfungaji.
Bao la tau la Simba SC na la mwisho katika mchezo a leo limefungwa na Mrundi Laudit Mavugo katika dakika ya 68 na kuishusha rasmi kileleni Yanga SC ambayo iko Moroni,Comoro kwa ajili ya michuano ya klabu bingwa Afrika.
Matokeo Mengine
Ruvu Shooting 0-0 Azam FC
Ndanda FC 0-0 Toto Africans
Mbao FC 0-0 Majimaji FC
0 comments:
Post a Comment