Osasuna,Hispania.
REAL MADRID imeendelea kujiwekea makazi ya kudumu kileleni mwa msimamo wa ligi ya La Liga baada ya usiku huu ikiwa ugenini Estadio El Sadar kuwafunga wenyeji wao Osasuna kwa mabao 3-1.
Cristiano Ronaldo alianza kuipatia Real Madrid bao la kuongoza katika dakika ya 24 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Karim Benzema lakini Sergio León aliisawazishia Osasuna baada ya kufunga bao la kusawazisha katika dakika ya 33 na kufanya timu hizo ziende mapumziko zikiwa zimefungana bao 1-1.
Kipindi cha pili kilikuwa kizuri zaidi kwa Real Madrid kwani ilijipatia mabao mwengine mawili yaliyofungwa na Isco katika dakika ya 62 pamoja na kinda Lucas Vázquez katika dakika ya 90'+ na kuifanya miamba hiyo ya Bernabeu ifikishe pointi 49.Pointi moja mbele ya Barcelona na pointi sita mbele ya Sevilla.Ikumbukwe Real Madrid ina michezo miwili pungufu.
Aidha katika mchezo huo Real Madrid na Osasuna zilipata mapigo baada ya walinzi wao Tano na Danilo kushindwa kumaliza mchezo kufuatia kupata majeruhi.
Matokeo mengine ya La Liga.
Real Betis 0-0 Valencia
Athletic Bilbao 2-1 Deportivo La Coruna
Michezo ya Jumapili
Villareal vs Malaga
Leganes vs Sporting Gijon
Las Palmas vs Sevilla
Atletico Madrid vs Celta Vigo
0 comments:
Post a Comment