Barcelona,Hispania.
MLINZI wa kulia wa Barcelona,Aleix Vidal atakosa michezo yote iliyosalia ya msimu wa 2016/17 kufuatia kuteguka kifundo cha mguu wake wa kulia katika ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Alaves jana Jumamosi.
Vidal mwenye umri wa miaka 27, alilazimika kutolewa uwanjani kwa msaada wa machela katika dakika ya 85 ya mchezo baada ya kugongana na winga wa Alaves,Theo Hernandez.
Barcelona imesema mlinzi huyo iliyemsajili mwaka 2015 kutoka Sevilla atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi mitano.
0 comments:
Post a Comment