728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, February 12, 2017

    Monaco yagonga mtu 5-0 Ufaransa,Falcao,Mbappe wapiga zote.

    Monaco,Ufaransa.

    MONACO imeendelea kukaza kamba kwenye mbio za ubingwa baada ya Jumamosi usiku ikiwa nyumbani Stade Louis II mbele ya watazamaji 6069 kuitungua Metz mabao 5-0 katika muendelezo wa michezo ya ligi daraja la kwanza Ufaransa maarufu kama Ligue 1.

    Nyota katika mchezo huo alikuwa ni kinda Kylian Mbappe,18, aliyefunga mabao matatu (hat-trick) katika dakika za 7 ', 20' na 50 '.

    Kwa kufunga mabao hayo matatu Mbappe amekuwa kinda wa kwanza kufunga idadi hiyo ya mabao baada ya Jeremy Menez aliyefunga idadi kama hiyo ya mabao mwaka 2005 akiwa na Sochaux.

    Mabao mengine ya Monaco yamefungwa na nahodha wake Radamel Falcao katika dakika za 10 na 55.Ushindi huo umeifanya Monaco ijikite kileleni baada ya kufikisha pointi 58 katika michezo 25.Nafasi ya pili inashilikiwa na PSG yenye pointi 55 katika michezo 25.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Monaco yagonga mtu 5-0 Ufaransa,Falcao,Mbappe wapiga zote. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top