728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, February 09, 2017

    Alichokisema Wenger baada ya kuripotiwa kumtaka Joe Hart.


    London,Uingereza.

    KOCHA wa Arsenal Mfaransa, Arsene Wenger amekanusha uvumi ulioenea siku ya jana kuwa anataka kumsajili kipa wa Manchester City aliyeko kwa mkopo Torino ya Italia, Mwingereza Joe Hart .

    Akifanya mahojiano na Arsenal.Com leo,Wenger amesema haoni sababu ya kumsajili Hart,27,kwani tayari anao makipa watatu wenye ubora wa dunia na ana furaha kubwa kuwa nao klabuni Arsenal.Petr Cech, David Ospina na Emiliano Martinez. 


    Wenger ametoa kauli hiyo baada ya jana Jumatano vyombo vya habari vya Uingereza kuripoti kuwa anataka kuachana na kipa wake namba moja Petr Cech baada ya Jumamosi iliyopita kufungisha bao moja katika kichapo cha mabao 3-1kutoka kwa Chelsea.

    Akimuongelea Cech, Wenger amesema "Kweli Cech alifanya kosa kwenye bao la tatu dhidi ya Chelsea lakini mbali na hayo amekuwa na msimu bora mpaka sasa.

    Cech alijiunga na Arsenal mwaka 2015 akitokea Chelsea kwa ada ya £10m na amebakisha miaka miwili kwenye mkataba wake.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Alichokisema Wenger baada ya kuripotiwa kumtaka Joe Hart. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top