728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, February 09, 2017

    Takwimu ligi kuu England: Watford,Man United zaongoza kwa madhambi

    Watford,Uingereza.

    WATFORD haipo kwenye zile timu nne za juu zinazowania ubingwa wa ligi kuu England msimu huu lakini linapokuja suala la timu inayoongoza kwa kufanya madhambi (fouls) miamba hii ya Vicarage Road iko juu ile mbaya.

    Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa hivi karibu zimeonyesha Watford inayonolewa na kocha Walter Mazzarri inashika nafasi ya kwanza katika orodha ya timu zilizofanya madhambi mengi zaidi msimu huu.Mpaka sasa Watford imefanya madhambi 346 ambayo yameonwa na mwamuzi na kuchukuliwa hatua.

    Nafai ya pili imeenda kwa Manchester United baada ya kufanya madhambi 322.Crystal Palace imeshika nafasi ya tatu ikiwa imefanya madhambi 311.

    Vilabu vya Chelsea,Arsenal na FC Bourmemouth vimeshika nafasi za 18,19 na 20 na vinasimama kama vilabu vilivyofanya madhambi machache zaidi ligi kuu England.

    Orodha Kamili
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Takwimu ligi kuu England: Watford,Man United zaongoza kwa madhambi Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top