728x90 AdSpace

Thursday, February 09, 2017

Pesa,mchezaji mmoja kutumika kumng'oa Shaw Man united.


London,Uingereza.

MAISHA ya beki wa kushoto wa Uingereza,Luke Shaw ndani ya Manchester United huenda yakakoma katika dirisha lijalo la usajili barani Ulaya hii ni baada ya  Tottenham kuripotiwa kuandaa ofa nono kuhakikisha beki huyo anayetumia vyema guu la kushoto anaondoka Old Trafford na kutua White Hart Lane.

Kwa mujibu wa mtandao wa Yahoo Sports taarifa zinasema kocha wa Tottenham,Muargentina Mauricio Pochettino anataka kuungana tena na Shaw baada ya kufanya nae kazi Southampton.

Katika kuhakikisha hilo linafanikiwa kwa urahisi Tottenham iko tayari kuipa Manchester United beki wake wa kushoto Danny Rose pamoja na pesa ili kumnasa Shaw ambaye amekuwa hana mahusiano mazuri na Kocha,Jose Mourinho.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: Pesa,mchezaji mmoja kutumika kumng'oa Shaw Man united. Rating: 5 Reviewed By: Unknown