Dar es Salaam,Tanzania
MABINGWA wa zamani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara,Simba SC wametangaza kumsajili aliyekuwa mlinzi wa Mwadui FC ya Shinyanga, Emmanuel Semwanza.
Semwanza mwenye uwezo wa kucheza kama mlinzi wa kulia,kati na kiungo amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuwatumikia wakali hao wa mtaa wa Msimbazi ikiwa imepita miezi mitano pekee tangu atue Mwadui FC katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo akitokea African Lyon ya Dar es Salaam.
Usajili wa Semwanza umekuja zikiwa ni siku chache tu tangu uongozi wa Simba SC utangaze kuwa uko katika mpango wa kukisuka upya kikosi chake kwa kusajili wachezaji wazawa.
0 comments:
Post a Comment