Bordeaux,Ufaransa.
BAO la dakika ya 81 la mshambuliaji Hal Robson Kanu limeipa Wales ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Slovakia katika mchezo mkali wa Kundi B uliochezwa katika uwanja wa Stade de Bordeaux huko Bordeaux.
Wales ndiyo walikuwa wa kwanza kuliona lango la Slovakia baada ya Gareth Bale kufunga dakika ya10 tu ya kipindi cha kwanza na kufanya mchezo uende mapumziko matokeo yakiwa 1-0.
Kipindi cha pili Slovakia walionyesha uhai na kuibana vilivyo Wales na kufanikiwa kupata bao la kufutia machozi dakika ya 61 kupitia kwa Ondrej Duda lakini dakika ya 81 Hal Robson Kanu aliifungia Wales bao la ushindi.
0 comments:
Post a Comment