Marseille,Ufaransa.
BAO la dakika ya 92 la nahodha Vasili Belezutski limeinyima England ushindi baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Urusi katika mchezo mkali wa Kundi B wa michuano ya Euro 2016 uliochezwa Jumamosi usiku katika uwanja wa Stade Veledrome ulioko Marseille.
England ndiyo walikuwa wa kwanza kufunga dakika ya 73 kupitia kwa kiungo wake Eric Dier,lakini nahodha Vasili Belezutski akaisawazishia Urusi dakika ya 92 na kufanya mchezo uishe kwa sare ya bao 1-1.
England itarejea tena dimbani Alhamis kuvaana na ndugu zao Wales huku Urusi wakicheza na Slovakia siku ya Jumatano.
VIKOSI
England: Hart, Walker, Cahill, Smalling, Rose,Alli, Dier, Rooney, Sterling, Kane, Lallana.
Akiba: Wilshere, Milner.
Russia: Akinfeev, Smolnikov, V.Berezutski,Ignashevich, Schennikov, Neustadter, Golovin,Kokorin, Shatov, Smolov, Dzyuba.
Akiba: Glushakov, Mamaev, Shirokov.
Mchezaji Bora wa mechi: Wayne Rooney
0 comments:
Post a Comment