Paris,Ufaransa.
USWISI imeianza vyema michuano ya Euro 2016 baada ya jioni ya leo kuwachapa majirani zao Albania kwa bao 1-0 katika mchezo mkali wa Kundi A uliochezwa katika uwanja wa Stade Bollaert-Delelis.
Bao pekee la mchezo huo
limefungwa dakika ya tano kwa kichwa na mlinzi Fabian Schar.Schar alifunga bao hilo akitumia makosa ya kipa wa Albania Etrit Berisha aliyeshindwa kuuwahi mpira wa kona uliopigwa na Xherdan Shaqiri.
Dakika ya 37 Albania ilipata pigo baada ya nahodha wake Lorik Cana kulimwa kadi nyekundu baada ya kushika mpira kwa maksudi.
Kwa matokeo hayo Uswisi imefikisha pointi tatu ikiwa sawa na wenyeji Ufaransa ambao jana Ijumaa waliifunga Romania kwa mabao 2-1 huko Stade de France.
0 comments:
Post a Comment