728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, June 11, 2016

    HIZI HAPA TAARIFA KUBWA ZA USAJILI TOKA ULAYA JUMAMOSI YA LEO JUNI 11,2016

    Afriyie Acquah

    Acquah:Kocha wa Manchester United Mreno Jose Mourinho ameripotiwa kuwa na mpango wa kutaka kuimarisha safu yake ya kiungo kwa kumsajili kiungo wa Torino Mghana Afriyie Acquah.Acquah,24,ambaye msimu uliopita aliifungia Torino mabao matatu katika michezo 31anadaiwa kuwa na thamani ya €12m. (Ghanasoccernet.com)

    Leandrinho:Manchester United imeripotiwa kuwa na nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji kinda wa Ponte Preta ya Brazil,Leandrinho,17, lakini huenda ikakabiliwa na upinzani mkali toka kwa wakala wa nyota huyo ambaye ameripotiwa kuwa na mpango wa kuona mteja wake akijiunga na Napoli kwa kuwa miamba hiyo ya Italia ina mipango mizuri na wachezaji vijana.(Radio CRC)

    Morata:Mshambuliaji wa Juventus Alvaro Morata,22, amedokeza kuwa atakuwa tayari kujiunga na Manchester United ikiwa tu Zlatan Ibrahimovic,34, hatajiunga na klabu hiyo ya jiji la Manchester.(Daily Mail)

    Cillessen:Everton imeonyesha nia ya kutaka kumsajili kipa wa Ajax Jasper Cillessen,27, kama mbadala wa kipa wake anayetaka kutimka klabuni hapo Mmarekani Tim
    Howard,34.Daily Telegraph )

    Pjanic:Wakala wa Miralem Pjanic amevipa matumaini vilabu vya Chelsea na Manchester United baada ya kukanusha uvumi ulionea nchini Italia kuwa mteja wake amefikia makubaliano ya kujiunga na Juventus.(Gazzetta )

    Zielinski:Liverpool imeripotiwa kutuma ofa ya €12m kwa ajili ya kutaka kumsajili kiungo wa Udinese Mpoland Piotr
    Zielinski ambaye pia anawaniwa na Napoli.(Sky Sports)

    Soares:Barcelona imemuongeza Cedric Soares wa Southampton katika orodha ya walinzi inaotaka kuwasajili ili kuziba nafasi ya mlinzi wake wa kulia Dani Alves anayetimkia Juventus. Mbali ya Soares,24, walinzi wengine wanaowindwa na Barcelona ni Hector Bellerin na Cesar Azpilicueta.(Mundo Deportivo )

    Toure:Wakala wa Yaya Toure anayeitwa Dimitri Seluk amesema anasubiri simu kutoka kwa mabosi wa Inter Milan ili aanze mpango wa kumuhamisha mteja wake kutoka Manchester City na kumpeleka Giuseppe Meaza.(Gazzetta )

    Bacca:Paris Saint Germain imeungana na Westham United katika mbio za kumuwania mshambuliaji wa AC Milan Mcolombia Carlos Bacca.Msimu uliopita Bacca, 29,aliifungia AC Milan mabao 18. (Gazzetta)

    Embolo: Manchester United imefungua mazungumzo na Basel kwa lengo la kutaka kumsajili mshambuliaji wake kinda Breel Embolowake,19,katika kipindi hiki cha majira ya joto.(Minuten)






    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIZI HAPA TAARIFA KUBWA ZA USAJILI TOKA ULAYA JUMAMOSI YA LEO JUNI 11,2016 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top