728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, June 05, 2016

    MWADUI FC YAZITEGEA YANGA,SIMBA

    Mwadui,Tanzania.

    Timu ya Mwadui ya Shinyanga, imesema haina mpango wa kuanza usajili wa wachezaji wake mapema kama ilivyo kwa timu zingine.

    Imesema lengo la kufanya hivyo ni kutaka kuwabaini wachezaji wangapi watakao ondoka katika klabu hiyo katika msimu ujao wa ligi kuu.

    Akizungumza jana, Kocha wa timu hiyo Jamhuri Kihwelu, alisema timu yake inasubiri kuona usajili wa timu kubwa za Yanga na Simba, ndipo nayo itachukua hatua.Dirisha la usajili linatarajia kufunguliwa rasmi Juni 25, mwaka huu.

    Hata hivyo, Julio alisema timu yake haina mpango wa kusajili wachezaji wengi kwa msimu ujao wa ligi.

    “Tunangojea kuona usajili wa timu hizo kubwa utakuwaje ili tujue ni wachezaji gani wataondoka na wapi wa kusajili,” alisema Julio.

    Alisema hawataki kuharakisha kusajili kwa sababu huenda timu kubwa zikaja kuwachukua wachezaji wao siku za usoni jambo litakalowapa wakati mgumu kuziba mapengo.

    “Tunaweza kusema tunasajili sasa, halafu baadaye kundi kubwa likaondoka na kutupa shida ya kuanza kutengeneza timu upya ndani ya muda mfupi,” alisema.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MWADUI FC YAZITEGEA YANGA,SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top