728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, June 05, 2016

    KUBWA ZA USAJILI TOKA ULAYA JUMAPILI YA LEO JUNI 5,2016 HIZI HAPA!!

    Erik Bailly


    Giroud:Mshambuliaji wa Arsenal Mfaransa Olivier Giroud amesema amezipokea kwa furaha habari za mshambuliaji wa Leceister City Jamie Vardy kukaribia kutua Emirates.Giroud,28,amesema usajili wa Vardy,27,utainufaisha sana Arsenal.Nimeambiwa Vardy anataka kujiunga na sisi,hiyo ni habari nzuri sana.Ni mchezaji mzuri,atatusaidia.(Sky Sports News HQ)

    N’Zonzi: Chelsea inataka kuimarisha safu yake na tayari imeripotiwa kuwa na mpango wa kumsajili kiungo wa Sevilla Mfaransa Steven N’Zonzi.N’Zonzi,27,aliyewahi kuvichezea vilabu vya Blackburn na Stoke City ametajwa kuwa na thamani ya £21m.(Daily Mirror)

    Schweinsteiger:Manchester United iko tayari kuuza kiungo wake Mjerumani Bastian Schweinsteiger ikiwa ni mwaka mmoja tu tangu imsajili toka Bayern Munich kwa ada ya £17m.
    (Daily Mirror)
     
    Wijnaldum:Vilabu vya Everton na Southampton vimeripotiwa kuwa jana Jumamosi vilituma maskauti wao kwenda kumtazama kiungo wa Newcastle United Georginio Wijnaldum,25,wakati akiichezea Uholanzi ilipokuwa ikivaana na Austria na kushinda kwa mabao 2-0.(Daily Mirror)

    Kante:Chelsea imedaiwa kuwa katika mazungumzo na kiungo wa Leceister City  N'Golo Kante kwa ajili ya kutaka kumsajili.Wakati huohuo taarifa kutoka Ufaransa zinasema kiungo huyo wa zamani wa Bolougne amesitisha mazungumzo hayo mpaka baada ya finali za Euro mwezi ujao.(beINSPORTS)

    Gibbs: Liverpool imeonyesha nia ya kutaka kuimarisha safu yake ya ulinzi baada ya kuripotiwa kutaka kumsajili mlinzi wa kushoto wa Arsenal Kieran Gibbs,26.Arsenal imeripotiwa kumuweka sokoni mlinzi huyo kufuatia kuwa na mpango wa kumsajili mlinzi wa kushoto wa Vfl Wolfsburg Mswisi Riccardo Rodriguez,23.( Football Insider )

    Bailly:Manchester United imeripotuwa kuwa katika hatua nzuri za kuinasa saini ya mlinzi wa Villarreal Muivory Coast Eric Bailly,22,kwa ada ya £32m.Mbali ya Manchester United vilabu vingine vilivyoripotiwa kumtaka mlinzi huyo mahiri ni Manchester City na Barcelona.( AS)

    Debuchy:Mathieu Debuchy ameripotiwa kuwa njiani kurudi Arsenal kupigania namba katika kikosi cha kwanza baada ya uhamisho wake wa mkopo katika klabu ya Bordeaux kufikia mwisho.Debuchy bado ana mkataba Arsenal mpaka 2019.(L’Equipe)

     Pellegrini:Meneja wa zamani wa Manchester City Manuel Pellegrini anatakiwa na Southampton ili kuchukua nafasi ya Meneja wa sasa wa klabu hiyo Ronald Koeman anayeelekea Everton.Koeman tayari ameshafikia makubaliano ya kuinoa Everton kwa mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya £21m.(Mirror)


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KUBWA ZA USAJILI TOKA ULAYA JUMAPILI YA LEO JUNI 5,2016 HIZI HAPA!! Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top