Mapou,Madagascar.
TIMU ya taifa ya Ghana maarufu kama Black Stars imekuwa timu ya tano kufuzu fainali za michuano ya Afrika (AFCON) mwakani baada ya leo mchana kuwafunga wenyeji wao Madagascar kwa mabao 2-0 katika mchezo wa Kundi H uliochezwa katika uwanja wa Anjalay huko Mapou,Madagascar.
Ghana ambayo iliingia katika mchezo wa leo ikihitaji sare yoyote ile iweze kufuzu imepata mabao yake kupitia kwa nahodha wake wa leo Andre Ayew dakika 70 na Christian Atsu dakika ya 74.Mabao yote mawili yametokana na krosi za mlinzi wa kushoto wa timu hiyo Baba Rahman anayechezea pia Chelsea ya England.
Kwa matokeo hayo Ghana imefuzu baada ya kufikisha pointi 13 ilizozipata katika michezo mitano,nafasi ya pili na ya tatu inashikiliwa na Rwanda pamoja na Msumbiji ambazo zote zina pointi sita kila moja.Madagascar ni ya mwisho ikiwa na pointi mbili pekee.
Timu ambazo zimefuzu mpaka sasa AFCON ni wenyeji wa michuano hiyo Gabon,Algeria,Cameroon, Senegal,Misri na Ghana.
0 comments:
Post a Comment