Madrid,Hispania.
Mlinda mlango wa FC Porto na timu ya taifa ya Hispania Iker Casillas Jumatano usiku aliweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyeichezea timu yake ya taifa michezo mingi zaidi kupita wachezaji wote Ulaya pale aliposhuka dimbani kuichezea Hispania katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Korea Kusini.
Katika mchezo huo ulioisha kwa Hispania kushinda kwa mabao 6-1,Casillas,32, alifikisha mchezo wa 167 akiwa na La Roja na kufanikiwa kumzidi Vitalijs Astafjevs wa Latvia mwenye michezo 166.
Casillas alianza kuichezea Hispania kwa mara ya kwanza Juni 3,2000 katika mchezo wa kimataifa wa Kirafiki dhidi ya Swedeni.Kabla ya hapo Casillas alivichezea vikosi vyote vya vijana vya Hispania vya U-15, 16, 17, 18, 20 na U 21.
Mpaka sasa Casillas ameishaiwezesha Hispania kutwaa kombe la dunia mwaka 2010 na kombe la Ulaya (Euro) mara mbili mwaka 2008 na 2012
0 comments:
Post a Comment