Brussels, Ubelgiji.
UBELGIJI imebanwa nyumbani na Finland baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo mkali wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa katika uwanja wa King Baudouin Stadium,Brussels.
Mchezo huo uliokuwa maalumu kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Ulaya [Euro 2016] inayotarajiwa kuanza Juni 10 mwaka huu ilishuhudia wageni Finland wakitangulia kupata bao la kuongoza dakika ya 53 kupitia kwa Kasper Hamalainan akitumia makosa ya mabeki wa Ubelgiji walioshindwa kuondosha hatari langoni mwao.
Mabadiliko yaliyofanywa dakika za mwisho na kocha Marc Wilmots kwa kumtoa Marouane Fellaini na kumuingiza Romelu Lukaku yalizaa matunda kwa Ubelgiji baada ya Lukaku kufunga bao la kusawazisha dakika ya 89 akiunganisha krosi ya Dries Mertens.
Katika mchezo mwingine wa kimataifa wa kirafiki Poland ikiwa nyumbani imeangukia pua baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Uholanzi huko Gdansk,Warsaw.
Mabao yaliyoipa ushindi Uholanzi yamefungwa na Vincent Janssen na Georginio Wijnaldum.Lile la Poland limefungwa na Artur Jedrzejczyk.
0 comments:
Post a Comment