Cairo,Misri.
TAARIFA za kuaminika toka Misri zinasema kwamba miamba ya soka ya nchi hiyo Al Ahly imevutiwa na mshambuliaji wa Yanga SC Mzimbabwe Donald Ngoma na iko tayari kumwaga pesa kumsajili.
Ngoma ambaye amekuwa na msimu mzuri sana tangu alipotua Yanga SC akitokea FC Platinum ya nyumbani kwao Zimbabwe amegeuka kivutio Al Ahly baada ya kufunga mabao 17 katika Ligi Kuu ya Vodacom,matatu katika Ligi ya Mabingwa Afrika likiwezo lile dhidi Wamisri hao na moja katika kombe la Ligi maarufu kama FA Cup.
Akifanya mahojiano hivi karibuni na Marwan Ahmed wa mtandao wa Kingfut.com,Ngoma amesema kuwa yuko tayari kutua Al Ahly.
"Kwanini hapana?Ni klabu kubwa Afrika na nitakuwa tayari kuhamia Misri ikiwa watanifuata"
“Why not? They are big side in Africa and I would be open to a move to Egypt”.
Al ahly imeripotiwa kuwa katika mpango wa kutafuta washambuliaji wapya wa kati baada ya kutoridhishwa na viwango vya washambuliaji wake wa sasa Malick Evouna kutoka Gabon na John Antwi kutoka Ghana.
0 comments:
Post a Comment