728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, June 19, 2016

    LIGI YA MABINGWA AFRIKA:SUNDOWNS,WAYDAD ZASHINDA UGENINI,MATOKEO YA MICHEZO YOTE YAKO HAPA

    SETIF,ALGERIA

    IKIWA ugenini Algeria,Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini imeianza vyema hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa Afrika baada ya Jumamosi Usiku kuichapa ES Setif kwa mabao 2-0 katika mchezo mkali wa Kundi B uliochezwa katika uwanja wa Stade du 8 Mai 1945 huko Setif,Algeria.

    Mabao ya Mamelodi Sundowns ambayo iliingia katika michuano hiyo baada AS Vita ya Kongo kutolewa kwa kosa la kuchezesha mchezaji asiye na sifa yamefungwa na Tiyani Mabunda (33) na Khama Billiat (63)

    Katika michezo mingine iliyochezwa Jumamosi toka Kundi A 

    Asec Mimosas ikiwa nyumbani katika dimba la Champroux stadium,Abidjan ,Ivory Coast imekubali kichapo cha bao 1-0 toka kwa Wydad Casablanca ya Morocco.Bao limefungwa na Salaheddine Saidi.

    Zanaco United ikiwa nyumbani Ndola,Zambia katika dimba la Levy Mwanawasa imeifumua Al Ahly kwa mabao 3-2.Mabao ya Zesco United yamefungwa na Clatous Chama aliyefunga mawili na George Ching'andu aliyefunga bao moja .Mabao yote ya Al Ahly yamefungwa na Mghana John Antwi.

     Michuano hiyo itaendelea tena leo Jumapili kwa mchezo mmoja wa kundi B kuchezwa ambapo Enyimba watakuwa nyumbani Port Harcourt,Nigeria kuivaa Zamalek ya Misri.

     

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: LIGI YA MABINGWA AFRIKA:SUNDOWNS,WAYDAD ZASHINDA UGENINI,MATOKEO YA MICHEZO YOTE YAKO HAPA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top