Aubameyang.
Pogba:Juventus imeripotiwa kujiandaa kuikataa ofa ya €120m kutoka Real Madrid kwa ajili ya kumuuza kiungo wake Mfaransa Paul Labile Pogba,23.(Mediaset Premium)
Falcao:Middlesbrough imeripotiwa kuwa na mpango wa kutaka kumsajili kwa mkopo wa miezi 12 mshambuliaji wa Monaco Mcolombia Radamel Falcao.Kocha wa Middlesbrough Aitor
Karanka ni rafiki mkubwa wa Falcao,31,hivyo anatarajia kutumia ukaribu huo kukamilisha dili hilo.(Daily Express)
Sarabia:Sevilla imeimarisha kikosi chake baada ya leo kuwasajili washambuliaji Pablo Sarabia kutoka Getafe na Mjapani Hiroshi Kiyotake kutoka Hannover.
Pjanic: Wakala wa kiungo wa AS Roma Miralem Pjanic,anayeitwa Adis Junuzovic amesema mteja wake yuko mbioni kujiunga na Juventus baada ya klabu hiyo ya Turin kukubali kupandisha ofa yake mpaka kufikia £30m.(Gazzetta dello Sport)
Sasha:Leicester City imeripotiwa kuungana na vilabu vya Arsenal na Manchester United katika mbio za kuiwania saini ya mshambuliaji wa kinda wa Internacional ya Brazil Eduardo Sasha.Sasha,18, ameifungia Internacional mabao sita msimu huu huku akiiwezesha kutwaa ubingwa wa jimbo la Gaucho.Sasha ameripotiwa kuwa na kipengele cha kuihama Internacional kwa ada ya €40m.(O'jogo)
Aubameyang:Borussia Dortmund imeripotiwa kuwa itaweka ngumu kumuuza mshambuliaji wake Pierre-Emerick Aubameyang kwenda Manchester City hata kama klabu hiyo ya jiji la Manchester itakuwa tayari kutoa ofa ya €70m kumsajili.(Bild)
Janssen:Tottenham Hotspur huenda ikakumbana na wakati mgumu katika kuinasa saini ya mshambuliaji wa AZ Alkmaar,Vincent Janssen,21, baada ya Wolfsburg kuripotiwa kuonyesha nia ya kumtaka nyota huyo aliyefunga mabao 32 msimu uliopita katika ligi ya Uholanzi Eledevisie.(BN DeStem)
Rodriguez:Vfl Wolfsburg imekubali kumuweka sokoni mlinzi wake wa kushoto Mswisi Ricardo
Rodriguez,23, baada ya staa huyo kuweka wazi nia yake ya kujiunga na Arsenal ambayo hivi karibuni ilimsajili rafiki yake wa siku nyingi Granit Xhaka.Rodriguez ataruhusiwa kuhama kwa ada ya £19m(Metro)
0 comments:
Post a Comment