Paris,Ufaransa.
UFARANSA imeianza vyema michuano ya Euro 2016 baada ya Ijumaa usiku kuifunga Romania kwa mabao 2-1 katika mchezo mkali wa ufunguzi wa Kundi A uliochezwa katika uwanja wa Stade de France,Paris.
Ufaransa ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 57 ya kipindi cha pili baada ya Olivier Giroud kufunga kwa kichwa safi.Giroud alifunga bao hilo akimalizia krosi ya Dimitri Payet iliyomshinda kipa wa Romania Ciprian Tatarusanu.
Dakika ya 65 Bogdan Stancu aliifungia Romania bao la kusawazisha kwa mkwaju wa penati.Penati hiyo ilitolewa na mwamuzi Victor Kassai baada ya Nicolae Stanciu kuangushwa ndani ya boksi na mlinzi wa kushoto wa Ufaransa Patrice Evra.
Mchezo ukiwa unaelekea ukingoni,dakika ya 89 Dimitri Payet aliifungia Ufaransa bao la ushindi kwa mkwaju mkali wa mguu wa kushoto na kufanya Ufaransa imetoke kifua mbele kwa mabao 2-1.
VIKOSI
Starting XI
France XI: Lloris; Sagna, Rami, Koscileny,
Evra; Matuidi, Pogba, Kanté; Payet,Giroud, Greizmann
Romania XI: Tătăruşanu, Săpunaru,Grigore, Chiricheş, Raţ, Hoban, Pintilii,Stanciu, Popa, Stancu, Andone
Ratiba ya leo Jumamosi Juni 11,2016.
Kundi A
Albania v Uswisi (16:00)
Kundi B
Wales v Slovakia (19:00)
England v Urusi (22:00)hh
0 comments:
Post a Comment