728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, June 11, 2016

    COPA AMERICA CENTENARIO:VIDAL APIGA ZOTE,CHILE IKIICHAPA BOLIVIA 2-1,MESSI APIGA 3 ARGENTINA IKISHINDA 5-0

    Foxborough,Massachusetts.

    MABAO mawili ya kiungo Arturo Vidal yameipa Chile ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Bolivia katika mchezo mkali wa kundi D uliochezwa katika uwanja wa Gillette huko Foxborough, Massachusetts.

    Vidal aliianza kuifunga Chile bao la kuongozA dakika ya 46 ya kipindi cha pili kabla ya Jhasmani Campos kuisawazishia Bolivia dakika ya 61 baada ya mkwaju wake wa faulo kumshinda kipa wa Chile Claudio Blavo na kutinga wavuni.

    Dakika ya 101 Vidal aliifungia Chile bao la pili kwa mkwaju wa penati uliopatikana baada ya beki wa Bolivia Luis Gutierrez kuunawa mpira ndani ya boksi.

    Kwa matokeo hayo Chile imefikisha pointi tatu baada ya kushuka dimbani mara mbili,Bolivia wao hawana pointi yoyote baada ya kupoteza michezo yote miwili.



    Katika mchezo wa pili wa kundi D,Argentina imeifunga Panama kwa mabao 5-0.Wafungaji Lionel Messi amefunga mbao matatu huku Nikolas Otamendi na Sergio Aguero wakifunga bao moja kila mmoja.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: COPA AMERICA CENTENARIO:VIDAL APIGA ZOTE,CHILE IKIICHAPA BOLIVIA 2-1,MESSI APIGA 3 ARGENTINA IKISHINDA 5-0 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top