Dar es Salaam,Tanzania.
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, imezidi kujitanua kimasoko na kuwafikia zaidi mashabiki wa soka nchini baada ya asubuhi hii
kuzindua uuzwaji wa vifaa vyake vya michezo kwenye boti zinazokwenda Unguja, Zanzibar.
Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Azam FC inayodhaminiwa na Benki ya NMB kuendeleza mradi wa uuzwaji bidhaa zake baada ya Mei 24 mwaka huu kuzindua duka kubwa la kuuza vifaa vyake vya michezo lililopo Mtaa wa
Mkunguni na Swahili,Kariakoo, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya vifaa hivyo ni pamoja na jezi, fulana, ‘track suit’, makoti ya mvua, kofia, soksi, raba za mazoezi,taulo, mipira, bendera, mabegi ya mgongoni na kusukuma, kalamu, vyote vikiwa na nembo ya klabu hiyo ambao ni mabingwa watetezi wa michuano
mikubwa ya Afrika Mashariki na Kati ngazi ya vilabu (CECAFA Kagame
Cup).
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa aina hiyo nyingine ya uuzaji wa vifaa
vyake leo ndani ya boti ya Azam Kilimanjaro (vi) , Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba,alisema
kuwa lengo kuu la kuuza jezi kwenye boti ni kuzidi kuwafikia mashabiki wa
timu hiyo na Watanzania kwa ujumla pamoja na kuongeza namba yao.
0 comments:
Post a Comment