Hassan Kessy.
Dar es Salaam,Tanzania.
MLINZI mpya wa kulia wa Yanga SC, Hassan Kessy Ramadhan anatarajiwa kuanza katika mchezo wa Kundi A wa hatua ya makundi ya kombe la shirikisho dhidi ya Mo Bejaia utakaofanyika Juni 17 huko Bejaia,Algeria.
Kessy amepewa jukumu hilo baada ya Juma abdul kuendelea kusumbuliwa na jeraha la kifundo cha mguu alilolipata katika mchezo wa fainali wa kombe la shirikisho dhidi ya Azam FC ulioisha kwa Yanga SC kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Abdul anatarajiwa kurejea tena dimbani baada ya wiki mbili kutoka sasa.
0 comments:
Post a Comment