Paris,Ufaransa.
CROATIA imeanza vyema michuano ya Euro 2016 baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Uturuki katika mchezo mkali wa Kundi D ulioisha hivi punde katika uwanja wa Parc des Princes,Paris.
Bao pekee la mchezo huo limefungwa dakika ya 41 na kiungo Luka Modric kwa mkwaju mkali wa umbali wa mita 25 na kumwacha kipa wa Uturuki Volkan Babacan akichupa bila mafanikio.
Kwa kufunga bao hilo Modric ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Croatia kufunga bao katika fainali mbili za Euro.Bao la kwanza alilifunga miaka minane iliyopita dhidi ya Australia.
Aidha bao hilo limekuwa ni bao la kwanza kwa mchezaji wa Croatia kufunga akiwa nje ya eneo la penati (Nje ya hatua18).Mabao yote yaliyofungwa kabla yalikuwa yakifungwa ndani ya eneo la hatua 18.
0 comments:
Post a Comment