Massachusetts,Marekani.
BRAZIL imetupwa nje ya michuano ya Copa America Centenario baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 toka kwa Peru katika mchezo mkali wa Kundi B uliochezwa katika uwanja wa Gillette Stadium, Foxborough,Massachusetts.
Bao pekee la mchezo huo limefungwa dakika ya 75 na Raul Ruidiaz.Rudiaz aliyekuwa ameingia akitokea benchi alifunga bao hilo kwa mkono akiunganisha pasi ya Andy Polo.
Kuingia na kukubaliwa kwa bao hilo kulimweka matatani mwamuzi Andres Cunha toka Uruguay baada ya wachezaji wa Brazil kumzonga na kumtaka afute bao hilo kwa madai mfungaji alitumia mkono kufunga.
Hii ni mara ya kwanza kwa Brazil kuondolewa katika hatua ya makundi ya michuano ya Copa America mara ya mwisho ilikuwa ni mwaka1987.
0 comments:
Post a Comment