728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, June 12, 2016

    HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI TOKA ULAYA JUMAPILI YA LEO JUNI 12,2016

    Edison Cavani

    Pogba:Juventus imeiambia Real Madrid imtoe kiungo wake Mjerumani Toni Kroos pamoja na kitita cha €120m ili iweze kupewa nafasi ya kumsajili kiungo wake Mfaransa Paul Pogba .(Marca)

    Ibrahimovic:Uhamisho wa mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic kwenda Manchester United huenda ukachelewa zaidi kukamilika baada ya staa huyo wa zamani wa Barcelona, Juventus na Inter Milan kuwa na mpango wa kuichezea Sweden katika michezo ya soka ya Olyimpiki.(Mirror)

    Schmeichel:Meneja mtarajiwa wa Everton Mholanzi Ronald Koeman ameripotiwa kuwa na mpango wa kutaka kumsajili kipa wa Leicester City Kasper Schmeichel ikiwa atashindwa kumsajili kipa wa Manchester City,Joe Hart.(Sunday People)

    Mercado:Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp ameripotiwa kuvutiwa na beki wa River Plate ya Argentina,Gabriel Mercado na huenda akatuma ofa ya £12m ili kumsajili.(Mirror)

    Mooy:Manchester City itamsajili kiungo wa Melbourne City,Aaron Mooy na kisha kumtoa kwa mkopo kwenda Ubelgiji.(Daily Star)

    Cavani:Baada ya Jamie Vardy kudengua Arsenal imeripotiwa kumgeukia mshambuliaji wa Paris Saint-Germain,Edinson Cavani ambaye hivi karibuni alikataa ofa ya mshahara wa £500,000 toka klabu moja ya China. (Express)

    Hysaj:Meneja wa Arsenal,Mfaransa Arsene Wenger amedaiwa kuvutiwa na mlinzi wa kulia wa Albania na Napoli, Elseid Hysaj na huenda akatuma ofa ya £12m ili kumsajili.Hysaj,22, pia anawindwa na Barcelona.(Daily Star)

    Zielinski: Liverpool imegonga mwamba katika mbio zake za kutaka kumsajili winga wa Udinese Piotr Zielinski baada ya staa huyo wa Poland mwenye miaka 22 kuripotiwa kuwa atajiunga na Napoli kwa ada ya €15m.(Gazzetta dello Sports)

    Ibe:Liverpool wameripotiwa kuwa na mpango wa kumtoa winga wake Jordan Ibe pamoja na pesa ili kuishawishi Southampton ikubali kumuuza winga wake Msenegal Sadio Mane,23.(The Sun)

    Allen:Liverpool wameiambia Swansea City itoe £10m ili iweze kuipata saini ya kiungo wake raia wa Wales Joe Allen.(Daily Mail)



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI TOKA ULAYA JUMAPILI YA LEO JUNI 12,2016 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top